Browser ni software application for retrieving, presenting and traversing information resources on the World Wide Web. Lakini pia inawezesha kucapture au kuinput taarifa ambayo inaweza kurudishwa kwa mfumo unaowasilisha, kisha kuhifadhiwa au kuchakatwa inapohitajika.
Hey, Mambo vipi, Leo tutazungumza kuhusu kugoogle au kutafuta majibu ya changamoto unapokuwa kwenye ujenzi wa mfumo. Je, unajisikia vibaya unapogoogle mambo kwenye mtandao kama programmer unanielewa nikisema Stack Overflow. Lakini je, kugoogle kunakufanya wewe kuwa programmer mbaya? Nitakueleza kwa uzoefu wangu pamoja na programmers mashuhuri kabisa ninaowafahamu ambao pia wameshare uzoefu wao katika hili. Nitakueleza pia kuna time unagoogle na hutapata kitu lakini kuna mtu unamjua ana uzoefu na sala unalohaingaika nalo, nakumbuka usemi wa waswahili, KUULIZA sio Ujinga. Hii ni Yesaya Software Podcast episode namba 34.
Leo tutazungumza kuhusu usalama wa taarifa za kibenki katika kufanya manunuzi online. Technolojia inabadilika kila leo, vilevile maarifa ya kulaghai watumia wa mitandao yazidi kuto tabirika. Mbinu mpya za udukuzi zinaibuka hivyo ni muhimu kutunza vizuri taarifa zako na kuwa makini na watu unaofanya nao biashara kwenye mtandao.
Leo tutazungumza uzoefu wangu katika kufanya manunuzi online sehemu ya pili. Kwenye toleo lilipita nilikueleza maandalizi niliyofanya kabla sijaagizo mzigo. Nilikueleza niliapanga kuagiza mzigo kupitia Amazon na eBay kutokana na maoni mbalimbali niliyopata. Pia njia ya kusafirisha mzigo kupitia MyUs.com na namna nilivyofunga sanduku la posta kiganjani kupitia SmartPosta.
Leo tutazungumza uzoefu wangu katika kufanya manunuzi online. Mid this year niliamua kufanya refresh ya tools ninatumia hapa Yesaya Software (camera, light and mixer) na nilitamani kufanya manunuzi online based on specific models ambazo nilipata recommendations kwa watu wengi online.
Leo nitakushikisha mambo ninayofanya nikiwa sina access ya Internet - yaani bundle limekata. Kwa kawaida nikiwa na internet na niko nyumbani kama siko na watoto basi muda mingi niko kwenye computer. Sometimes sina mood ya kazi basi hapo ndio ninapoteza muda kwenye magroup na Twitter huko. Ila bundle limekata, ninafanya nini? Nitafurahi kusikia pia kutoka kwako, kuna rafiki yangu mmoja amenijubu, baada ya kummuliza anafanya nini bundle likikata, ameniambia ananunua bundle.
Hey, Mambo vipi, Leo nitakupatia update ya kazi niliyofanya this weekend. Nimekamilisha kurekodi na kupublish video 8 kuhusu Laravel Community Website. Na kubwa tunatengeza website hii pamoja, hakikisha unachek kule GitHub kuweza kushiriki ujenzi na pia kule YouTube kwa video tutorials kuhusu development ya hii website. Lakini kabla hatujasonga mbele ninapenda kuchukua fursa hii kukushukuru sana kwa kuweza nifanikisha kufikia download elfu 5 kwenye Yesaya Software Podcast. It means a lot kwangu na wewe ni modaux mkubwa kwenye hili. Asante. Hii ni Yesaya Software Podcast episode no 29.
Leo tunakwenda kujadili kidogo kuhusu path niliyochukua kutengeneza cross platform apps, hapa ninamaanisha Android and iOS App. Kutokea awali nimekuwa mzito sana kudevelop apps ambazo sio native yaani sio specific kwa Android na iOS. Nina imani toleo hili litakuwa msaada pia kwa wadau mbalimbali wa TEHAMA kujua technolojia zinazohusika kutengeneza Mobile Apps.
Ukweli na Elimu kuhusu YouTube Monetisation
Leo kwenye Twitter Spaces na Yesaya Software tumejadili kuhusu uhusiano wa Mentor na Mentee. Tulijadili mambo mengi ikiwa na kuangalia sababu za kwa nini utahiji mentor.